Jangili
$4.99
Balaa linaibuka usiku wa fungate, maharusi wakiwa ndani ya chumba cha hoteli walichoandaliwa. Wanavamiwa na Bwana harusi kujeruhiwa vibaya huku Bibi harusi akichukuliwa na watu. Likiwa ni tukio la ajabu ambalo linaacha wengi midomo wazi
Bwana harusi ni kijana wa familia ya kitajiri hapo mjini. Familia yake inahaha hasa kumsaka mkewe sambamba na kuwajua wabaya waliyofanya tukio lile la kinyama lililofanya akafanyiwe upasuaji hatari.
Wapelelezi wawili, ASP Kawambwa na Norbert Kaila wanalivalia njuga suala hilo kulichunguza. Ndipo wanakuja kujua kuna uwepo wa jangili nyuma ya kila kitu. Ndiye aliyefanya mchezo ule, akiwinda mali kiharamu.
Contacter le commerçant pour commander :